habari Mpya


Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale yapokea zaidi ya shilingi milion 67 kwaajili ya ujenzi.Geita na Gibson Mika

Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita imepokea vifaa vya ujenzi kwa awamu ya kwanza vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 67 na laki nane kutoka kampuni ya uchimbaji wa madini ya Dhababu ya Acacia kupitia  mgodi wa Bulyanhulu kwa lengo la kukamilisha ujenzi wa maboma ya zahanati 10 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi zao kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi vifaa hivyo lililofanyika katika kijiji cha Nyang’holongo Kata ya Nundu Mkoani Geita, Meneja mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu amesema wanatarajia kuendelea kuwaunga mkono wananchi katika ukamilishaji wa maboma ya zahanati Mbalimbali na kwamba zaidi ya milioni mia tano zimekwisha tengwa kwa ajiri ya zoezi hilo.
Bw,Busunzu amesema kuwa vifaa vyote vya ujenzi vinatarajiwa kununuliwa katika maduka ya wafanyabiashara walio ndani ya wilaya hiyo kwa lengo la kuwaunga mkono wafanya biashara pia.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale Bi mariam Chaulembo amewataka wananchi kuhakikisha wanaweka ulizi wa kutosha katika vifaa hivyo ili viweze kufanya kazi iliyokusudiwa ya kukamilisha zahanati hizo kwa wakati na kuwasaidia wananchi hasa akina mama wajawazito wazee na watoto kuepukana na changamoto ya kutembea mwendo mrefu wakitafuta huduma za matibabu.
Nao baadhi ya wananchi wa kijiji cha nyang’holongo wamesema wamekuwa wakilazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 20 wakitafuta huduma za matibabu katika kituo cha afya cha kharumwa na kwamba kukamilika kwa zahanati hiyo itakuwa neema kwao.
Post a Comment

0 Comments