Mkuu wa Mkoa GAGUTI katika hafla hiyo fupi aliziagiza Mamlaka
za Serikali za Mitaa kuhakikisha zinakusanya takwimu za Wafanyabiashara wote
Wakubwa, wa Kati na wale Wadogo ifikapo Februari 15, 2019 takwimu hizo ziwe
zimewasilishwa ofisini kwake lengo likiwa ni kuhakikisha kila mwananchi
anayetoa bidhaa yoyote na kupokea fedha anatambuliwa na kulipa kodi au tozo stahiki
za Serikali.
|
Hafla hiyo fupi iliyowashirikisha Wakuu wa Wilaya saba za
Mkoa wa Kagera, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa,
Wenyeviti wa Halmashauri na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba, Watendaji wa
Kata wa Manispaa ya Bukoba waliowawakilisha Watendaji wenzao katika mkoa ambao
walitakiwa kutoa changamoto zinazowakumba katika ugawaji wa vitambulisho vya
Wafanyabiashara Wadogo katika maeneno yao.
|
Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Wakitoa changamoto mbalimbali
kuhusu ugawaji wa vitambulisho Watendaji wa Kata walisema kuwa changamoto
kubwa ni Elimu kwa wananchi kutojua ni mfanyabiashara yupi anatakiwa kupata
kitambulisho na ni yupi hastahili kupata na changamoto hiyo inatokana na suala
la mauzo ghafi kutoeleweka vizuri kwao wao wenyewe Watendaji kama wahusuika wa ugawaji lakini pia
wafanyabiashara jambo ambalo waliitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
kutoa uelewa kwao.
Changamoto nyingine iliyotajwa na Watendaji wa Kata
waliohudhuria hafla fupi ya kukabidhi vitambulisho kwa Wakuu wa Wilaya ni suala la Mfanyabiashara Mdogo kuwa na namba ya
utambuzi ya mlipa kodi ya TRA (TIN) wakati biashara yake ni ndogo na hastahili
kupata kitambulisho cha mfanyabiashara mdogo wakati mtaji wake ni mdogo
haufikii kiwango cha shilingi milioni 4,000,000/= kwa mwaka.
Akitoa majibu ya changamoto
zilizowasilishwa na Watendaji wa Kata Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa
wa Kagera Bw. ADAM NTOGA alisema kuwa Mfanyabiashara Mdogo anayestahili kupata
kitambulisho ni yule ambaye mauzo yake kwa siku hayafikii shilingi 11,000/= kwa
siku. Kama Mfanyabiashara anauza bidhaa zake na kupata kiwango cha fedha chini
ya shilingi 11,000/= huyo anastahili kupata kitambulisho cha Mfanyabiashara Mdogo.
“Hata kama Mfanyabiashara
ana mtaji wa shilingi 5,000/= lakini anauza bidhaa zake kwa siku na kupata
shilingi 11,000/= au zaidi kwa siku huyo hastahili kupata kitambulisho,
kinachoangaliwa hapa si mtaji wa mfanyabiashara alionao bali ni mauzo yake kila
siku kama anapata kiasi cha shilingi 11,000/= au chini ya kiwango hicho.”
Alifafanua Bw. Adamu Ntoga
Katika huatua nyingine Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa onyo kwa
Wafanyabiashara ambao walidanganya na kupokea vitambulisho wakiwa tayari
wametambuliwa na mfumo wa ulipaji kodi wa TRA kuwa tayari anayo amajina sita
hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwao mara moja.
Pia aliwaonya Watendaji wa
Kata ambao wanaandika barua kuwatambulisha wafanyabiashara kuwa mtaji wao ni
mdogo kuwa waache mara moja.
“Watendaji wa Kata acheni hizo tabia zenu za kuwaandikia
barua wafanyabiashara na kuwatambulisha kuwa biashara zao ni ndogo, kama kuna
Mfanyabiashara alipita TRA na kujisajiliwa mwacheni apite huko huko na kufanyiwa
tathimini upya na TRA wao ndiyo watoe barua hizo vinginevyo mkiendelea hatua
zitachukuliwa kwenu.” Alionya Mkuu wa Mkoa Gaguti.
Aidha, Mkuu wa Mkoa alitoa ufafanuzi juu ya
Wafanyabiashara Wadogo wanaopata vitambulisho kuendelea kutoa tozo ndogo ndogo
za Halmashauri husika katika maeneo wanayofanyia biashara mfano tozo za
kukusanya taka au huduma za vyoo na usafi na kuwataka kutotumia kigezo cha
vitambulisho na kuacha kulipa tozo hizo.
Pia Wafanyabiashara ambao tayari
wanatakiwa kulipa kodi katika Halmashauri wanatakiwa kuendelea kulipa kodi hizo
baada ya kufanyiwa tathimini na TRA.
Mkoa wa Kagera katika awamu ya kwanza ulipatiwa vitambulisho
vya Wafanyabiashara Wadogo 25,000 na Wilaya ya Bukoba ilipatiwa jumla ya
vitambulisho 3,580. Wilaya za Missenyi, Karagwe, Kyerwa, Ngara, Muleba, na
Biharamulo zilipatiwa vitambulisho 3,570 kila moja.
Hadi tarehe 1 Februari,2019
vilikuwa vimegawiwa vitambulisho 16,369
sawa na asilimia 65% kwa Wilaya zote na kiasi cha shilingi milioni 327,380,000/=
zilikuwa zimekusanywa na kupelekwa benki.
Vitambulisho vya awamu ya pili Mkoa wa Kagera
ulipatiwa vitambulisho 35,000 na vitambulisho hivyo vimegawiwa katika Wilaya
kulingana na Jiografia ya Wilaya, wingi wa watu na hali ya kiuchumi tofauti na
awamu ya kwanza ambapo katika awamu ya pili Wilaya Bukoba iligawiwa
vitambulisho 7,000 Biharamulo na Ngara kila moja iligawiwa vitambulisho 4,200.
Kyerwa na Missenyi kila moja vitambulisho 4,400 na Wilaya za Karagwe na Muleba
ziligawiwa vitambulisho 5,400.
|
0 Comments