habari Mpya


Habari picha mazishi ya Padre Raphael Nyabenda KakwavuNgara Picha na Samuel Lucas/Habari na Amina semagogwa
Mwili wa aliyekuwa Padre Raphael Nyabenda Kakwavu wa Parokia ya Nyakato Ddekania ya Chato Jimbo katoliki la Rulenge Ngara umeagwa leo katika kanisa la Yesu kristo mfalme Parokia ya Rulenge jimbo katoliki la Rulenge Ngara.


Akiongoza Ibadaya misa takatifu ya kuuga mwili huo, makam wa Askof Monsinyori Padre Barnabas Sumbuso amesema jimbo limepata pigo kubwa la kuondokewa na mpendwa wao katika shamba la bwana.

 
Amesema kifo cha padre Raphael Nyabenda Kakwavu nifundisho kwa kila muumini kujiweka tayar wakati wote kwani hakuna anayejua siku wala saa ya kuitwa kwake mbinguni

Padre Raphael Nyabenda Kakwavu alifariki jumamosi usiku wakati akipatiwa matibabu katika Hospital teule ya wilaya ya Biharamlo

Post a Comment

0 Comments