habari Mpya


DC na DED Biharamulo Waonywa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza Mkuu wa wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera, -Sada Malunde na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Wende Ng’ahara kumaliza tofauti zao na wasipojirekebisha atamshauri Rais John Magufuli kufanya maamuzi mengine.

 Amesema kuwa kitendo cha viongozi hao kutoelewana kinaonesha mfano mbaya kwa watumishi walio chini yao, hivyo amewataka kuacha tabia hiyo mara moja.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa onyo hilo wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira wa shule ya msingi ya Nyakanazi wilayani Biharamulo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Kagera.

Amesema kuwa kutoelewana kwa viongozi hao ambao wakati mwingine wanatuhumiana kufanyiana vitendo vya kishirikina, kumesababisha kuzorota kwa shughuli za maendeleo katika wilaya hiyo ya Biharamulo.

Post a Comment

0 Comments