habari Mpya


Bilioni 48.8 Kutumika kwenye Miradi ya Maendeleo Kasulu Mwaka 2019/2020.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akipewa maelezo ya Ujenzi wa Kituo cha  Afya Kiganamo katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu,  Mkoani Kigoma, kutoka kwa Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, Dkt. Mshana Dastan, alipotembelea na kufanya ukaguzi wa Kituo hicho.

Picha na Maktaba yetu.
Baraza la Madiwani wa Halamshauri ya wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma limepitisha Mapendekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2019/2020 yenye zaidi ya shilingi bilioni 48.8 kwa ajili ya maendeleo ya halmashauri hiyo. 

Akiwasililisha Bajeti hiyo, Afisa Mipango wa halmashauri Bw. JACCOBO KILATU amesema ili kukidhi mapendekezo hayo halmshauri inatarajia kukusanya kiasi hicho kutoka Serikali kuu na Mapato ya ndani ya halmashauri hiyo. 

Bajeti hiyo imejielekeza zaidi katika Elimu, Afya na Maji kwa kukamilisha miradi ambayo haijakamilika na miradi mingine mipya iliyoibuliwa na wananchi katika kata 21 za halmashauri hiyo. 

SIKILIZA ZAIDI HAPA RIPOTI YA ALBERT KAVANO.

Post a Comment

0 Comments