habari Mpya


Baraza la mawaziri lapigilia Msumari wamwisho katika Ujenzi wa mradi wa umeme wa mapromoko ya mto Ruvubu

Baraza la mawaziri kutoka Tanzania, Rwanda na Burundi limeiagiza bodi ya wakurugenzi wa mradi wa maporomoko ya umeme wa Rusumo mkoani Kagera kukamilisha Mradi huo ifikapo mwezi Februari mwaka 2020

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye ni waziri wa Nishati nchini Tanzania Dakt. Medard Kalemani amesema serikali ya Tanzania, Rwanda na Burundi zimeafikiana kutoa maagizo hayo ili mradi huo ukamilike kwa wakati

Aidha Dakt. Kalemani amesema mradi huo ukikamilika uatazalisha Megawati 80 za umeme ambapo nchi hizo zitagawana Megawati 27 kila moja

Mawaziri wengine waliokuwepo ni waziri wa Nishati na Nadini wa Burundi Mhandisi Come Manirakiza na Balozi Cleva Gatete waziri wa Miundo mbinu wa Rwanda na wameazimia kukutana kabla ya mwezi June mwaka huu kuangalia maendeleo ya mradi huo


Mradi wa Umeme wa maporomoko ya Mto Rusumo umeanza mwaka 2015 na unafadhiliwa na Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Africa


Balozi Cleva Gatete waziri wa Miundo mbinu wa Rwanda
Post a Comment

0 Comments