habari Mpya


Yanga SC waifumua Mwadui FC Ligi Kuu Tanzania bara.

Yanga SC wameendeleza ubabe na kupata ushindi wa magoli 3-1,kwenye mechi yake ya Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga, nyumbani uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Magoli ya Yanga SC yakipatikana kupitia kwa Ibrahim Ajib dakika ya 12, Amissi Tambwe dakika ya 39 na Feisal Salum dakika ya 58 wakati Mwadui FC wameambualia goli moja lililofungwa na Salim Aye dakika ya 82.

Yanga SC sasa baada ya kupata ushindi huo inazidi kujikita kileleni na kuwafanya wafikishe pointi 53 wakikamilisha michezo yao ya mzunguuko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania bara 2018/2019, wakati Azam FC wakiifuatia Yanga SC kwakuwa na pointi 40 ila wana viporo vya mechi  mbili leo January 16,2019 wakicheza na Ruvu Shooting, wakati Simba SC wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi 33 wakiwa na viporo vya michezo mitano.

Post a Comment

0 Comments