habari Mpya


Waziri Ndalichako –Mwisho Jumatano wiki hii Waliokula Fedha za Elimu Bure.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa JOYCE NDALICHAKO ametoa siku mbili (JUMATANO JANUARY 30, 2019 ) kwa Watumishi wa Elimu kote nchini waliokula fedha za elimu bure kuzirejesha mara moja.

Waziri NDALICHAKO amesema “Kila nikitazama habari mpaka inakera kila mtu analalamika ujenzi wa madarasa mnamwambia nani? huo ni uzembe wenu”.

 “Siwezi nikafurahia pesa yeyote inayopita kwenye mikono yangu nataka mrudishe fedha mtazitoa wapi hayatuhusu, nitampasia Jafo yeye atafunga goli” Waziri NDALICHAKO.

MSIKILIZE HAPA WAZIRI JOYCE NDALICHAKO NA TAMKO LAKE KUHUSU FEDHA ZA ELIMU BURE NCHINI.

Post a Comment

0 Comments