habari Mpya


Watu Nane Watuhumiwa wa Ujambazi Wauawa Katika Majibizano ya risasi na Askari Kigoma.

Watu nane wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi wameuawa katika majibizano ya risasi na askari wa Jeshi la polisi Mkoani Kigoma kwenye pori la Muyovozi Wilayani Kakonko.

 Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kigoma Martin Ottieno amesema kuwa katika tukio hilo, mbali na kuuawa kwa watuhumiwa hao, polisi pia wamekamata bunduki moja aina ya AK 47 ikiwa na risasi Kumi.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kigoma, – MARTIN OTTIENO amezungumza na Mwanahabari wetu SAMUEL LUCAS ailetaka kujua undani wa Tukio Hilo.

WAWEZA SIKILIZA HAPA MAHOJIANO YA KAMANDA WA POLISI WA MKOA WA KIGOMA.

Post a Comment

0 Comments