habari Mpya


Wanawake Washauriwa Kumuogopa Mungu Na Kufuata Sheria Za Nchi


Na Shaaban Ndyamukama.
Wanawake wameshauriwa kumuogopa mungu na sheria za nchi kwa kuepuka vitendo vya ukatili dhidi ya watoto baada ya kuwapata kwa kuwazaa kisha kuwaua au kuwatelekeza wakiwaacja mazingira hatarishi.

Ushauri huo umetolewa na mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Ngara mkoani Kagera Witness Mwanga baada ya kuungana na wenzake kutembelea watoto yatima wa kituo ANGEL'S HOME kilichopo Kanisa katoliki la Rulenge wilayani Ngara.
Witness Mwanga amesema kuzaa mtoto ni baraka hivyo mtoto anahitaji malezi, matunzo na kupewa haki zake za msingi kuliko kumtupa na kumsababishia maisha magumu akilelewa na watu wengine
"Sisi tungetelekezwa au kuuawa leo tusingeliweza kuwatembelea watoto hawa wanaohitaji msaada mkubwa, wito wangu kwa wazazi ogopeni Mungu na mamlaka zilizo juu yenu kuwapa watoto haki ya kuishi"Alisema Mwanga
Pichani kulia aliye beba mtoto ni wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Ngara mkoani Kagera Witness Mwanga.

Baadhi ya wafanyakazi hao wa NMB tawi la Ngara wametoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Shilingi 340,000 ambapo  meneja wa huduma kwa wateja NMB  Bw. Meleck Manyama amesema vitu hivyo ni vyakula vinywaji mavazi kidogo, sabuni  mafuta na vifaa vya kujifunzia kwa wanaosoma shule.

Amesema wao kama sehemu ya jamii wamechangishana na kupata kiasi hicho kisha kuungana na watoto hao kuwapatia gawio la mapato  mfano wa sadaka wakianza mwaka mpya 2019.

" Kwa mazingira tuliyoyaona wanavyoishi unahitajika msaada zaidi kutoka kwa watu mbalimbali kuweza kuwapa moyo walezi ambao ni masista wa kanisa na kwa jinsi wanavyowahudumia Mungu awabariki"Amesema Manyama
Nao watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Angle's home wametoa Shukrani zao kwa zawadi walizopokea huku wakinyanyua mikono kuwaombea kwa Mungu wakijawa na furaha,wakicheza na kuimba.

Pia mkuu wa kituo cha Angle's home Sir Mariagholeth Felix amesema watoto wanaolelewa kituoni hapo ni wenye umri wa miezi  sita mpaka miaka  20 ambao walipatikana baada ya mama zao kufariki kwa kujifungua au kuokotwa.

Pamoja na kushukuru watu mbalimbali wanaofika kutoa msaada kwa watoto amesema kituo hicho kinao watoto 47 wanaotoka sehemu mbalimbali  kama Ngara karagwe Chato, na Kahama na kwamba wanafundishwa malezi ya kiroho hadi wanapokua na kujitambua.

Picha.Sista Veronica Hamwi akiwaonesha wafanyakazi wa NMB tawi la Ngara mkoani Kagera watoto wanaolelewa katika kituo ANGEL'S HOME kilichopo Kanisa katoliki la Rulenge wilayani Ngara
Post a Comment

0 Comments