habari Mpya


Uhaba wa Vyumba vya Madarasa Kasulu waathiri Wanafunzi 1845 kutoripoti Shule.

Mkuu wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Kanali Simon Anange akikabidhi vitabu vya stakabadhi kwa Watendaji wa kata za Halmashauri ya Mji wa Kasulu , kwa ajili ya kukusanyia fedha za michango ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 46 shule za Sekondari.
Jumla ya wanafunzi 1845 wa kidato cha kwanza wilayani Kasulu mkoani Kigoma,huenda wakashindwa kuripoti shuleni kutokana na shule walizopangiwa kuwa na uhaba wa vyumba vya madarasa.


Hali iliyo walazimu viongozi wa wilaya kwa kushirikiana na wananchi kujenga Vyumba 46 vya madarasa ili wanafunzi hao waliopangiwa katika shule za sekondari waripoti.


Kanali Simon Anange ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kasulu, ameongeza  madarasa hayo yatatakiwa kujengwa kwa nguvu za wananchi na serikali kuchangia mabati pamoja na ukarabati wa vyumba hivyo.

Post a Comment

0 Comments