habari Mpya


Walimu Missenyi Wampongeza Rais Magufuli kwa Kufuta Kikokotoo.

Na Anord Kailembo –RK Misenyi.

Walimu wilayani Missenyi mkoani Kagera wameandamana hadi kwa Mkuu wa wilaya hiyo, kupeleka barua ya kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuhairisha kikokotoo cha kanuni mpya ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii.

Kiongozi wa msafara huo, Katibu wa Chama cha Walimu wilayani Missenyi Mwl. Rosemery Mboneko amesema kuwa walimu wamefurahishwa na maamuzi ya busara yaliyofanywa na Rais Magufuli na kwamba wanaamini kitakapomalizika kipindi cha mpito yatakuja maamuzi mengine ya busara.

Aidha ameiomba serikali kama iliyothamini mchango wa watumishi katika suala la kikokotoo, Ifanyie kazi changamoto zinazowakabili ikiwemo kutokupandishwa madaraja na kupewa fedha za likizo kwa wakati pamoja na changamoto ya uhaba wa walimu.
Moja ya Bango wakati wa Maandamano.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Misenyi, Kanal Denis Mwila amesema kuwa Serikali iliyoko madarakani inatetea maslai ya watanzania wote bila ubaguzi na kuwataka walimu hao kuwa wavumilivu wakati serikali ikiendelea kufanyia kazi changamoto zinazowakabiri.

Post a Comment

0 Comments