habari Mpya


Vijana Dogeza Foundation Watoa Laki 3 Kusaidia Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa 37 Buhigwe,Kigoma.

Mkuu wa wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma Luten Kanal Michael Ngayalina akipokea mchango wa shilingi Laki 3 na kipaza sauti kimoja kutoka kwa Kikundi cha VIJANA DOGEZA FOUNDATION ,kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 37 ili Wanafunzi 1,229 waliokosa nafasi ya kuendelea na masomo ya sekondari mwaka huu 2019 waendelee kati ya wanafunzi 3,031 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wilayani humo.

Na Philmon Golkanus –RK Buhigwe 94.2.
Kikundi cha VIJANA CHA DOGEZA FOUNDATION kikionesha mfuko ulio na  mchango wa shilingi  Laki 3 walizozitoa kwa  Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya vijana hao kuunga mkono juhudi za serikali katika ujenzi wa madarasa kwa ajili ya wanafunzi waliokosa nafasi ya kuendelea na elimu ya sekondari.

Kutoka Wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma Mwanahabari wetu PHILLEMON GOLKANUS anasimulizi yake hapa chini sikiliza kwa kubofya Play.

Post a Comment

0 Comments