habari Mpya


Tamko la Naibu Waziri wa Kilimo Kuhusu Kahawa ya Mkulima Kagera.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa.
Wizara ya Kilimo imesitisha Madeni yote yaliyokuwa yanadaiwa na vyama vya ushirika Mkoani Kagera ambavyo ni chama Kikuu cha Ushirika KDCU LTD cha  wilaya  za  Karagwe na Kyerwa, KCU   na NGARA FARMARS hadi pale maelekezo na utaratibu mwingine utakapotolewa na WIZARA.

 Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo  ambaye  pia ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe Mhe.Innocent Luga Bashungwa wakati akiongea na vyombo vya habari ambapo alikuwa akitoa mrejesho wa hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Wizara ya jinsi wakulima wa kahawa watakavyo nufaika na zao hilo.
BOFYA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA.
Mhe.Bashungwa ametaja moja ya sababu za kusitisha madeni hayo kuwa imetokana na mapato yanayopatikana kupitia vyama vya ushirika baada ya uuzaji wa kahawa wanalipwa wadeni kabla ya wakulima wenye mali.

Post a Comment

0 Comments