habari Mpya


TAKUKURU yamkamata Mfanyabiashara wa Simu Bandia Geita.

Na Gibson Mika –RK Geita 90.5

Taasisi ya Kuzuwia na kupambana na Rushwa Mkoa wa Geita imefanikiwa kumkamata mfanya biashara wa vifaa vya simu kutokana na kuingiz bidhaa kimagendo na kufanya biashara.


Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake, Mkuu wa TAKUKURU THOBIAS NDARO amesema baada ya kufanya uchunguzi na ufuatiliaji wa taarifa za mfanyabiashara huyo Bw. Ombary Njovu wamefanikiwa kumkamata na kumchukulia hatua za kisheria.

Hata hivyo, amewataka wafanyabiashara kufanya biashara kwa kuzingatia sheria za nchi kwa kutoa risiti kwa wateja wao na kwamba kwa kipindi cha miezi mitatu, zaidi ya shilingi Milioni 15 zimeokolewa kutoka kwa wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi.

MSIKILIZE HAPA CHINI-BOFYA PLAY

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa mkoa wa Geita wamewataka wafanyabiashara kuacha kukwepa kulipa kodi ili kuleta maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa.

Post a Comment

0 Comments