habari Mpya


Stori 4Yaliyojiri :Tetea Ukatili kwa Wanaume,Elimu duni kwa Wajasiriamali Kigoma,Ugumu wa Maisha Ngara na Biashara ya Nyama Yadoda Biharamulo.

MWANZA RK 97.7

Wanaharakati wa haki za binadamu  katika mataifa mbalimbali wameshauriwa kukemea  ukatili wa kijinsia kwa kutetea  Wanaume wanaofanyiwa vitendo vibaya na wanawake ndani ya familia kuleta usawa wa haki  mbele ya sheria.


Ushauri huo umetolewa na Mkufunzi wa chuo cha Ualimu Butimba Mwalimu AGUSTINE KASASE wakati akiongea na Mwanahabari wetu SHAABAN NDYAMUKAMA.
  

BOFYA KITUFE CHA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA ZAIDI.
KIGOMA UJIJI RK 94.2
Imeelezwa kuwa mwamko kwa baadhi ya wafanyabiashara na Wajasiriamali mkoani Kigoma katika kurasimisha biashara zao bado ni mdogo hali inayosababisha washindwe kutambuliwa na serikali.
Kutoka Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma Mwanahabari wetu ADRIAN EUSTACE anasmulizi zaidi.
BOFYA KITUFE CHA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA ZAIDI.
NGARA RK 97.9
Ugumu wa maisha kwa baadhi ya familia katika jamii umekuwa ukisababisha wanafamilia kushindwa kupata mahitaji ya muhimu hasa pale wanapopatwa na matatizo yanayohitaji fedha ili kuyatatua.
Baadhi ya familia hizo zimekuwa zikiamua kukaa kimya kwa kudhani kuwa hazina pakukimbilia ili kupata msaada.
Mwanahabari wetu Sr OLIVA NIYONZIMA amefika katika kijiji cha Murukukumbo wilayani Ngara mkoani Kagera, na kutuandalia makala fupi.
BOFYA KITUFE CHA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA ZAIDI.
BIHARAMULO 97.9
Baadhi ya wafanyabiashara wa nyama ya ng`ombe na mbuzi wilayani  Biharamulo mkoani Kagera wamelazimika kufunga bucha kwa kile kinachodaiwa kukosekana kwa walaji.
Kutoka Wilayani Biharamulo Mkoani Kagera Mwanahabari wetu WILLIAM MPANJU anataarifa zaidi.
BOFYA KITUFE CHA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA ZAIDI.

Post a Comment

0 Comments