habari Mpya


Shule ya Msingi Kihinga yapata ufadhili baada ya kuadhiriwa na Bomu mwaka 2017.

Pichani ni mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Luteni Kanali Michael Mangwela Mtenjele.
Shule ya Msingi Kihinga iliyopo wilayani Ngara mkoani Kagera imepata ufadhili wa vyumba viwili vya madarasa,ofisi ya walimu na madawati 30 vyenye  thamani ya shilingi milioni 76 kufuatia shule hiyo kuathiliwa na Bomu Novemba 2017 na kusababisha wanafunzi watano kufariki na wengine 43 kujeruhiwa.


Ufadhili huo umetolewa na shirika la Tumaini Fund lililopo wilayani Ngara mkoani Kagera ambapo Mratibu  wa taasisi hiyo Alex Nyamkara akiambatana  na Mwenyekiti wa mfuko huo Dakt.Suzan Wilson kutoka nchini Uingereza wamekabidhi miundombinu hiyo kwa shule hiyo baada ya tukio la bomu lililoharibu madarasa manne

Nyamkara  amesema licha ya vyumba hivyo, wakati wa tukio taasisi hiyo ilitoa msaada  wa matibabu yaliyogharimu Sh6 milioni  kwa wanafunzi waliojeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya  misheni Rulenge wilayani Ngara.

Pichani ni Jengo ambalo limejengwa na Tumaini Fund


Pichani ni Dakt.Suzan Wilson kutoka nchini Uingereza ambaye ndiye amefadhili ujenzi wa miundombinu hiyo chini ya mfuko wa Tumain wilayani Ngara.
Pichani ni jengo la shule ya msingi Kighinga ambalo liliathiriwa na Bomu.

Post a Comment

0 Comments