habari Mpya


Serikali Biharamulo Kuboresha Sekta ya Kilimo 2019 Kwa Kujenga Ghala la Kuhifadhia Chakula.

Na Wiliam Mpanju –RK Biharamulo.

Serikali ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera imepanga kuboresha sekta ya kilimo kwa mwaka 2019 kwa kuwajengea ghala la kuhifadhia chakula ili kuwezesha wakulima kuuza mazao yao kwa bei ya soko la uhakika.


Mkuu wa wilaya ya Biharamulo Bi. Saada Malunde amesema ghala hilo litajengwa katika eneo la Lusahunga kwa ajili ya kutunzia mazao ya Wakulima.

Amesema kwa muda mrefu wakulima wa Biharamulo wamekuwa wakilalamikia kukosa soko la mazao, hivyo Serikali ya wilaya ina mpango madhubuti wa kumtafutia soko na kumnufuashia Mkulima.
Baadhi ya Wakulima wa kata ya Ruziba, Lusahunga na Bisibo wamesema kila wakivuna mazao yao hasa mahindi, maharage na mihogo hawapati soko la uhakika jambo ambalo limekuwa likiwakatisha tamaa na kulazimika kuuza mazao yao kwa bei ya rejareja katika magulio ya kawaida.

Post a Comment

0 Comments