habari Mpya


RC Mongella Akagua Ujenzi Hospitali ya Bwisya Ukerewe.

Na Maria Philbert -RK Mwanza 97.7
Mkuu wa Mkoa Mwanza JOHN MONGELLA amekagua upanuzi wa Kituo cha Afya Bwisya kilichopo katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe, kinachojengwa kwa hadhi ya Hospitali ya Wilaya. 

Itakumbukwa kwamba Novemba 17 mwaka jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, SELEMANI JAFO alizindua rasmi ujenzi wa miundombinu katika Kituo hicho unaofanywa na kampuni ya SUMA JKT chini ya usimamizi wa Kamati Maalum iliyoundwa na Mongella kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 800. 
Huu ni utekelezaji wa agizo la Rais DKT. JOHN MAGUFULI aliyeagiza sehemu ya fedha za rambirambi zilizopatikana kufuatia ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere kilichozama Septemba 20 mwaka 2018 zitumike kufanya ukarabati katika Kituo cha Afya Bwisya ili kuboresha huduma za afya kwa wakazi wa kisiwa cha Ukara.
WAWEZA KUMSIKILIZA HAPA CHINI KWA KUBOFYA PLAY.

Naye msimamizi wa mradi wa ujenzi wa kituo cha afya kutoka Suma JKT Luteni KHAMIS MASOUD amesema kuwa mradi wa upanuzi wa Kituo cha Afya Bwisya unatarajia kukamilika mwezi Februari mwaka huu na utagharimu shilingi milioni 856 na tayari wameshajenga majengo 8 ambayo yamefikia hatua ya kuezeka.

Post a Comment

0 Comments