habari Mpya


Mwekezaji Kutoka Korea Kusini Kuineemesha Ngara kwa Miradi hii Mikubwa ya Maendeleo.


Mwekezaji kutoka   Korea Kusini amewasili kwa mara ya pili wilayani Ngara mkoani Kagera, nakuahidi kujenga kituo cha Afya katika  kijiji cha Kazingati kata ya Keza anakotegemea kuanzisha miradi ya kiuchumi wilayani Ngara.

Mwekezaji huyo Kim Won Dae ametoa ahadi huyo January 14,2019 baada ya kutembelea eneo atakalowekeza kilimo cha kahawa na mpunga na kujenga kiwanda cha kukoboa na kusaga zao hilo kisha kujenga kiwanda cha mbolea.
Kituo hicho kitajengwa kwa thamani ya Shilingi milioni 250 za Kitanzani sambamba na kujengwa shule ya kimataifa   (international school ) itakayogharimu Shilingi milioni 600  katika  mamlaka ya mji mdogo wa Rulenge kwa kuwekewa vifaa vya aina mbalimbali kuandaa wataalamu wa kisayansi.

Taarifa ya Mwanahabari wetu SHAABAN NDYAMUKAMA kutoka Wilayani Ngara  inasomwa na SWAUMU JUMA kutoka Chumba chetu cha Habari.

BOFYA KITUFE CHA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA ZAIDI.

Post a Comment

0 Comments