habari Mpya


Muleba Yagawa Kitambulisho Cha Mjasiriamali Mdogo.

Mkuu wa wilaya ya Muleba mkoani Kagera ,Mhandisi RICHARD RUYANGO akikabidhi Vitambulisho 3570 vya Wafanyabiashara Wadogo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya wilaya  hiyo Bw. EMMANUEL SHEREMBI kwa ajili ya kuwagawia wafanyabiashara wadogo Wilayani Muleba Mkoani Kagera ili wafanye biashara zao bila usumbufu.

Na Shafiru Yusuf –RK Muleba 97.7.
Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhandisi RICHARD RUYANGO akimvalisha JOANITHA JULIUS Kitambulisho cha Mjasiriamali Mdogo katika uwanja wa fatuma mjini Muleba baada ya kukidhi vigezo.
Mhandisi RICHARD RUYANGO.

 Akizindua ugawaji wa vitambulisho hivyo hivi karibu, Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhandisi RICHARD RUYANGO katika uwanja wa fatuma wilayani humo,amesema kuwa vitambulisho hivyo vitagawiwa katika kata zote za wilaya hiyo kwa wajasiriamali wadogo waliokidhi vigezo vya kupatiwa vitambulisho hivyo.

Mhandisi RUYANGO pia amewaagiza watendaji wa kata zote pamoja na Maafisa Biashara  wilayani humo kutoa elimu kwa wajasiriamali hao ili waweze kupatiwa vitambulisho hivyo na wafanye biashara zao kwa uhuru na kuongeza kuwa wajasiriamali wadogo walioko maeneo ya visiwani na kata nyingine zilizoko mbali watafuatwa katika maeneo yao ili kuepusha usumbufu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya wilaya  hiyo Bw. EMMANUEL SHEREMBI.
Naye meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania wilaya ya Muleba Bw.Mohamed Kapela amesema mjasiriamali ambaye atapewa kitambulisho hicho ni Yule ambaye anamauzo ya chini ya MILIONI NNE kwa mwaka na kitambulisho hicho kinalipiwa shilingi elfu ishirini tu.

Kwa upande wao baadhi ya wajasiliamali waliopatiwa vitambulisho hivyo EVERIUS SARVATORI NA JOANITHA JULIUS wamesema wataondokana na adha waliyokuwa wanaipata hapo awali kabla ya kupatiwa vitambulisho hivyo na wanaimani watafanya biashara zao kwa amani.

Post a Comment

0 Comments