habari Mpya


Muhimu Serikali Kurasimisha Biashara ya Wajasirimali Wadogo Nchini –Dkt.Mramba.

Kitambulisho Cha Mjasiriamali Mdogo.

Desmba 10, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli  akiwa Ikulu Jijini Dar es Salaam alitoa vitambulisho vya Wajasiriamali wadogo 670,000 kwa Wakuu wa Mikoa yote na kila Mkoa ulipatiwa vitambulisho 25,000 ambapo Rais Magufuli alisema lengo ni Wafanyabiashara hao Wadogo waweze kufanya shughuli zao za ujasiriamali na kujiingizia kipato chao cha kila siku bila kusumbuliwa na mtu yeyote.
Na Erick Ezekiel- RK Sengerema 97.7.

Serikali imetakiwa kuboresha mazingira ya wafanyabiashara wadogo nchini ili kurasimisha biashara hiyo na kuongeza vyanzo vya mapato kupitia ukusanyaji wa kodi.

Akizungumza na Radio Kwizera, Mtafiti wa Masuala ya Wajasiriamali Wadogo na Mhadhili wa Chuo cha CBE jijini Mwanza Dkt. Nassib Rajab Mramba amesema licha ya serikali kuendelea kugawa vitambulisho kwa wajasiriamali hao ipo haja ya kutazama upya mazingira ya biashara zao.

Dr.Mramba amesema kinachokosekana kwasasa ni sera na mfumo rafiki kwa wafanya biashara hao ili kurasimisha biashara zao.

MSIKILIZE HAPA -Dkt.MRAMBA.


Nao baadhi ya machinga waliozungumza na radio kwizera wamesema huenda ikawa ahueni kwa sasa baada ya serikali kuwatambua kwa kuwapa vitambulisho na kwamba utaratibu wa ukusanyaji kodi kutoka kwao unafaa kuendana na mazingira ya biashara.

Post a Comment

0 Comments