habari Mpya


Mtibwa Sugar yapigwa 2-0 Tanzania Prisons Ligi Kuu.

Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar jioni ya January 8,2019 kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya ikiwa ni mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara  2018/2019.

Ushindi huo wa kwanza chini ya kocha mpya MOHAMMED ‘ADOLPH’ RISHARD aliyechukua nafasi ya MOHAMMED ABDALLAH ‘BARES’ aliyefukuzwa baada ya matokeo mabaya umetokana na mabao ya Salum Kimenya dakika ya 71 na Jumanne Elfadhil dakika ya 88.
 
Kwa ushindi huo unaifanya Tanzania Prisons ifikishe pointi 15 baada ya kucheza mechi 20 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 19 kutoka ya mwisho, ya 20.

Post a Comment

0 Comments