habari Mpya


Matokeo Ligi Kuu Tanzania Bara 2018/2019 Mzunguko wa 19.

Kocha Amri Said ‘Stam’.

 Timu ya Biashara United chini ya Kocha wao mpya Amri Said ‘Stam’ imepata alama 3 muhimu baada ya kocha huyo kuiongoza timu hiyo kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania bara mzunguko wa 19.

Ushindi huo wa kwanza tu wa kocha Amri Said tangu ajiunge na timu hiyo juzi akitokea kwa majirani, Mbao FC ya Mwanza umetokana na mabao ya Daniel Manyenye dakika ya 18 na Juma Mpakala dakika ya 20, wakati bao la Mbeya City limefungwa na Frank Ikobela dakika ya 26.

Biashara United iliyopanda Ligi Kuu msimu huu 2018/2019, inafikisha pointi 13 katika mechi ya 18 baada ya ushindi huo, ikipanda kwa nafasi moja hadi ya 19 ikiiteremshia mkiani Tanzania Prisons, nafasi ya 20.

MECHI NYINGINE ZA LIGI KUU LEO HAPA CHINI MATOKEO YAKE KAMILI.

Post a Comment

0 Comments