habari Mpya


Maafisa wa Kambi za Wakimbizi Kigoma Wasimamishwa Kazi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewasimamisha kazi baadhi ya maafisa wa Idara ya Huduma kwa wakimbizi baada ya hivi karibuni kukamatwa kwa marobota yenye sare 1,947 za kijeshi katika kambi mbili za wakimbizi mkoani Kigoma.

Kukamatwa kwa sare hizo kulitangazwa Ijumaa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Samson Anga baada ya kukamatwa kwa nguo hizo katika kambi za wakimbizi za Nduta wilayani Kibondo na Mtendeli, Wilaya ya Kakonko.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Jumapili, Waziri Lugola amesema amechukua uamuzi huo kutokana na maafisa hao kutokufuatilia kwa umakini uingizwaji wa marobota hayo yaliyokuwa na nguo za msaada kwa ajili ya wakimbizi.

Post a Comment

0 Comments