habari Mpya


Kubwa 3 za Yaliyojiri -Elimu Lishe Kasulu,Kamati ya Maji Kibondo na Uhaba wa Vyoo Muleba.

KASULU.
Imeelezwa kuwa Elimu ya lishe inayotolewa na serikali kwa kushirikiana na Mashirika na asasi za Kiraia, Jamii wilayani Kasulu imeonesha mabadaliko ya tabia za jamii na kuelekea mafanikio ya kupunguza Udumavu wilayani humo.


Kutoka Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma Mwanahabari wetu ALBERT KAVANO anataarifa zaidi.
KIGOMA.
Kamati ya maji na usimamizi wa mazingira na maliasiri katika kijiji cha Rusohoko wilayani kibondo mkoani kigoma imepanda miti rafiki wa maji katika vyanzo vya maji vya kijiji hicho ili kutunza mazingira na vyanzo vya maji vinavyoonekana kuanza kukauka kutokana na shughuli za kibinadamu.
Mwanahabari wetu JAMES JOVINE anataarifa zaidi kutoka Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma.
MJI MDOGO WA MULEBA.

Uhaba wa vyoo vya kudumu katika shule za msingi Wilayani Muleba Mkoani Kagera umetajwa kuwa chanzo cha utoro kwa baadhi ya wanafunzi hali inayopelekea kushuka kwa taaluma mashuleni.

Kutoka Wilayani Muleba Mkoani Kagera Mwanahabari wetu SHAFIRU YUSUPH anataarifa zaidi.

Post a Comment

0 Comments