habari Mpya


Eneo la Uwekezaji Kazingati Ngara lazua Mgogoro Kati ya Wananchi na Viongozi wa Kisiasa.

Askari Polisi wakiimalisha Usalama kwenye Mkutano wa Hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Ngara mkoani Kagera Mhe. Alex Gashaza kijijini Kazingati.

Na Shaaban Ndyamukama –RK Ngara 97.9.

Mbunge wa Jimbo la Ngara mkoani Kagera Mhe.Alex Gashaza (CCM) amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Kazingati katika jimbo hilo chini ya vyombo vya ulinzi na usalama, baada ya kuwepo malalamiko ya kwamba anapinga wawekezaji kupata ardhi kijijini humo.

 Mbunge huyo  Gashaza amefanya mkutano huo January 2, 2019  ikiwa ni siku chache Katibu mkuu wa Chama  Cha Mapinduzi  ngazi ya Taifa kuagiza uongozi wa wilaya ya Ngara kuacha mara moja mipango ya kugawa ardhi kwa mwekezaji kutoka korea Kusini.

Wawekezaji wa nchi hiyo wanahitaji ardhi  kwa ajili ya kilimo  cha kahawa na mpunga pia kujenga kiwanda cha Kahawa na mbolea na wamesaini mkataba wa kupewa ekari 12,000 kutoka kijiji cha Kazingati wilayani Ngara licha ya viongozi wa kijiji hicho kuridhia ardhi yenye ukubwa wa ekari 1000.
Mhe.Alex gashaza.

Katika mkutano huo wananchi wamepinga hoja ya Mbunge kwamba, haukufuatwa utaratibu wa kugawa ardhi ya kijiji hicho kwa wawekezaji kutoka Korea Kusini.

Wamesema kwamba wanaridhia wawekezaji wa taifa hilo kuanzisha miradi ya maendeleo wajipatie ajira kujikwamua kiuchumi huku wakidai ardhi iliyopo ni maeneo ya wazi hawanufaiki nayo ukiachilia malisho ya mifugo.
Mmoja wa wananchi wa kijiji hicho Mathayo Daniel amesema  ardhi hiyo imejaa ng’ombe wanaotoka kwa wafugaji wa nje ya kijiji hicho wakiwemo raia wa nchi jirani lakini wananchi hawanufaiki ispokuwa viongozi  hivyo ardhi wawekezaji waruhusiwe kuanzisha miradi yao

Sisi wananchi wa kijii cha Kazingati tuliitwa na  Mwenyekiti wa kijiji, akatuuliza kuhusu kugawa ardhi tulimkubalia na kuhitaji kupata ajira na lakini pia ardhi iliyopo katika kijiji hiki inatosha  kuwekeza unapinga  wawekezaji lini tutapata ajira na kufaidika?” Alihoji Daniel

Naye Johanseni Rumuli amewatuhumu viongozi kugawa ardhi bila wananchi kushirikishwa na hivi sasa baadhi ya maeneo ya wakulima na wafugaji yamewekewa alama za watu ambao wanatumia ardhi hiyo bila kuridhiwa na mkutano mkuu wa kijiji na serikali ya wilaya hiyo.
Askari Polisi wakiimalisha Usalama eneo la Mkutano.

Mbunge wa Ngara Mhe.Alex Gashaza  anapinga kutolewa ardhi kwa wawekezaji wa Korea Kusini baada ya kusainiwa mkataba (MOU) wa kuchukua ardhi ekari 12,000 wa kati wananchi   hawakuridhia katika mkutano wa hadhara  na ardhi ya kijiji hicho ukubwa wake ni ekari 8,000.  

Aidha madai ya Mbunge huyo ni kwamba hakuna kikao cha  Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara kilifanyika kupitisha  kugawa ardhi ya kijiji cha Kazingati ambayo ilibainishwa kwenye vitongoji vya vya Muko  na Msalasi vyenye ukubwa usiozidi ekari 4,140.

"Mkurugenzi wa halmashauri aliomba ekari 1000 katika kijiji hicho lakini mkataba wa wakezaji wamesaini ekari 12,000 kitu kinachoashiria ukiukaji wa taratibu kwa sheria ya ardhi namba tano ya mwaka 1999" Amesema Gashaza.
Ramani ya Eneo la Uwekezaji kijiji cha Kazingati,Ngara mkoni Kagera.

Mwenyekiti wa  Halmashauri ya Ngara,Mhe. Erick Nkilamachumu amesema, utaratibu wa kitoa ardhi ulifuatwa na malengo ni wananchi kupata miradi kujiongeea mapato kiuchumi.

Amesema matarajio ya halmashauri ilikuwa kupata waeekezaji kuunga mkono juhudi za serikali za tanzania kuwa na uchumi wa kati na viwanda ambapo hata wilaya ya ngara ingesonga mbele katika kukusanya mapato

"Mgogoro huo hadi halmashauri iufikishe   wizara ya ardhi kwa waziri mwenye mamlaka ndiye atakayeweza  kuutolea ufafanuzi badala ya kujibia hoja mkanganyiko sijichonganishi na wananchi ".Amesema Nkilamachumu

Mgogoro huo wa ardhi ya kijiji hicho umesababisha mgawanyiko wa wananchi na viongozi wa kisiasa baina  yao na Mbunge huyo  Alex Gashaza, pia kuwepo dalili za  ukabila baina ya Wahangaza wa Bugufi anakotoka Mbunge huyo na kabila la washubi ilipo ardhi ya hao wawekezaji.

Post a Comment

0 Comments