habari Mpya


Askofu Bendankeha- ''2019 Hasira na Chuki tuiache na Tuishi Maisha ya Amani na Utulivu''.

Askofu wa kanisa kuu la Anglikan Dayosis ya Kagera Darlington Bendankeha.

Na Shaban Ndyamukama –RK Ngara 97.9.

Askofu wa kanisa kuu la Anglikan Dayosis ya Kagera Darlington Bendankeha amewataka watanzania kusahau mambo magumu  waliyopitia mwaka 2018 na kumuomba Mungu kuwalinda katika Amani na Utulivu  kwa mwaka  2019.

Askofu Bendankeha amesema hayo ndani ya Kanisa kuu la Murugwanza wilayani Ngara, katika ibada ya mkesha wa Mwaka Mpya 2019 na kwamba matukio mengi ndani ya jamii   yamejitokeza na kusononesha nyoyo za watu.

Amesema nafasi ya mwaka uliopita 2018 iwe nafasi ya kutafakari mambo magumu yaliyopita kwa kuwa upendo umepungua na huu ni wakati wa mabadiliko.

Katika ibada hiyo wachungaji,  wanaume na wanawake waliopewa nafasi  yakutoa maombi  malum kwa Mungu kumbariki  Rais Dkt. John Pombe Magufuli kufanya kazi  kwa heshima na weledi wakiwemo  watendaji walio chini yake.

Post a Comment

0 Comments