habari Mpya


Watu wawili Wamefariki na Wengine11wamelazwa Hospitali baada ya Kuangukiwa na Ukuta wa kanisa-Kahama.


Watu wawili wamefariki na wengine11wamelazwa katika hospitali ya mji wa Kahama Mkoani Shinyanga baada ya kuangukiwa na ukuta wa kanisa wakati wakifanya mazoezi ya kwaya .

Wakizungumza na Radio Kwizera baadhi ya majeruhi waliolazwa katika hiospitali ya mji wa Kahama waumini wa kanisa la Waadiventista Wasabato, wamesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11 jioni ambapo ilinyensha mvua yenye upepo mkali na kusababisha ukuta kubomoka.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi katika hospitali ya mji wa Kahama Dr George Masasi amekiri kupokea miili ya watu wawili ambao ni Judiness Ngusa mwenye miaka 37 na Mtoto Elisha Masai mwenye miaka 5 na kati ya majeruhi hao wanawake wako nane na wanaume watatu na hali zao zinaendelea vizuri.

Jeshi la Polisi wilayani Kahama limekiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba taarifa za awali zinaonesha ujenzi wa kanisa hilo ulikuwa haujakamilika licha ya kwamba walikuwa wakilitumia kwa ajili ya ibada.

Post a Comment

0 Comments