habari Mpya


Wananchi wa Kijiji cha Buhororo wataka Ulinzi Uimarishwe Baada ya Bendera ya Kijiji Kuibwa.

Mkutano wa Kijiji Ukiendelea.

Na  Shaaban Ndyamukama –RK Ngara.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya vijana wamemvamia askari mgambo na kumpora bendera ya Taifa inayotumika katika ofisi ya kijiji cha Buhororo  wilaya ya Ngara mkoani Kagera  na kuondoka nayo.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Staford Simon amesema bendera hiyo ilichukuliwa na vijana wanaosadikiwa kuishi   kijiji hicho  na kwamba  askari wa mgambo  alikuwa akiipeleka bendera hiyo nyumbani baada ya kuishusha kutoka kwenye mlingoti wa ofisi ya kijiji SAA 12:30 siku kadhaa zilizopita.
Amesema hayo jana December 5,2018 jioni kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa dharura kujadili hali ya ulinzi na usalama na kwamba waliohusika walitolewa taarifa katika kituo cha polisi makao makuu wilayani Ngara kwa uchunguzi zaidi.

Alisema baada ya taarifa hiyo watuhumiwa waliitwa polisi kutoa maelezo kasha walipewa dhamana lakini baadaye waliileta bendera na kuitelekeza kwenye ofisi ya kijiji.

Ameeleza kuwa baada ya kupatikana ikiwa imetelekezwa,vyombo vya ulinzi na usalama vineichukua bendera hiyo kwa upelelezi zaidi.
 Jeshi la polisi wilayani Ngara limethibitisha kuibiwa kwa bendera hiyo  na kwamba baada ya kupokea taarifa za vingozi wa kijiji linafanya upelelezi kujiridhisha na ikibainika ukweli wake vijana wanaotuhumiwa watafikishwa mahakamani.

Katika hatua nyingine, Wananchi wa kijiji hicho wameomba ulinzi uimarishwe ili kuimarisha usalama kwani kumekuwa na wimbi la wizi mdogo mdogo ikiwemo ndizi shambani, kubomoa nyumba na vifaa vya magari.

Post a Comment

0 Comments