habari Mpya


Wafanya biasha soko kuu Biharamulo mjini wakerwa na kizimba cha taka kilicho jaa bila kuzolewa.

BIHARAMULO NA SHAABAN NDYAMUKAMA
Takataka zilizojaa kwenye dampo la soko kuu  la Biharamulo mkoani Kagera zimeanza kutoa harufu mbaya na huenda zikasababisha magonjwa ya mlipuko kwa wanaokaa jirani na soko hilo kama takataka hizo hazitaondolewa mapema.

Watumiaji wa soko hilo ambao ni wajasiriamali  wamesema uchafu na mizoga inasambaa maeneo mbalimbali ya vibanda vya wafanya biashara na kuwa kero katika mji wa Biharamulo lakini viongozi wa halmashauri hawajachukua hatua kuboresha mazingira hayo kiafya

Mwenyekiti wa soko hilo la Biharamulo mjini Hassan Said Kisangani na katibu wake Venelabris Keizilahabi wamesema changamoto iliyopo ni ukosefu wa gari la kuzoa taka kutoka ofisi ya Mkurugenzi mtendaji na kusababisha takataka hizo kukaa kwenye dampo muda mrefu

Hata hivyo Afisa usafi na Mazingira wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo  Michael  Mkuti kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya a Biharamulo amesema gari limeishapatikana na uchafu huo utaondolewa kuanzia wiki hii lakini pia wafanyabiashara wa soko hilo  washiriki kutunza mazingira.

Post a Comment

0 Comments