habari Mpya


Wabadilisha Fedha mpakani Wilaya ya Ngara Watakiwa Kujisajili ili Kutambulika Kisheria.

Na Shaaban Ndyamukama -RK Ngara 97.9

Wafanyabiashara  wa kubadilisha fedha  katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera  wameshauriwa  kujisajili ili kutambulika kisheria. 

Kaimu Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Forodha Kabanga wilayani Ngara Seifu Mkilindi ametoa ushauri huo hivi karibuni mbele ya  waandishi wa habari Ofisini kwake na kwamba usajili huo lazima uanzie na mwenye kuwa na dola elfu  10 na kuendelea kwa mujibu wa sheria, kupitia benki kuu  ya Tanzania BOT na shirika la fedha duniani IMF.

 Amesema  kwa upande wa Tanzania wanaofanya biashara ya kubadilisha fedha  ni wachache katika kituo cha Kabanga hawapo ispokuwa raia wa Burundi wanaofanya biashara hiyo kwa kujificha katika mpaka wa Kobero.

Serikali ya Tanzania katika kufuata taratibu za kibiashara wanekuwepo wanaojihusisha na huduma hii wanelazimishwa kuijisajili kulipia kodi na kuongeza mapato  na kufanya shughuli kihalali” Alisema Mkilindi.

Aidha baadhi ya wateja waliotoka Tanzania na Burundi katika mpaka wa kobero mpakani mwa Tanzania na Burundi wamesema  kubadilisha fedha kunategemea na kiwango cha kupanda au kushuka kwa dola katika soko la kimataifa.

Hata hivyo baadhi ya vijana wa Ngara na Rwanda wameonekana kituo cha Forodha Rusumo wakibadilisha fedha kwa kuwapatia abiria  wakiwemo madereva wanaiongia na kutoka  mataifa hayo  kuelekea nchi ya  Kongo DRC.

Post a Comment

0 Comments