habari Mpya


Utafiti Kuja na Aina mpya ya Ndizi kumaliza Utapiamulo Kagera.

Aina mpya ya ndizi kumaliza utapiamulo Kagera.

Katika jitihada za kuhakikisha kwamba tatizo la utapiamlo na udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano linamalizwa nchini, utafiti umeanza kufanywa mkoani Kagera ili kupata mbegu bora zinazotoa ndizi zenye vitamin`A’.


 Kituo cha Utafiti Maruku kimeanza kufanya utafiti wa aina 9 za migomba zinazotoa ndizi zenye vitamin`A’ zikiwemo aina 3 za migomba ya asili zinazolimwa katika mkoa wa Kagera.

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la chakula duniani za mwaka 2015 /2016 zinaonyesha mkoa wa Kagera kuwa miongoni mwa mikoa 10 iliyo na kiwango kikubwa cha udumavu kwa watoto.

Mkuu wa Idara ya Migomba katika kituo cha utafiti Maruku Dkt. Mpoki Shimwera anasema kuwa wameamua kufanya majaribio ya migomba hiyo ili kuweza kupata migomba itakayokubalika kwa wakulima pamoja na walaji wa ndizi lengo likiwa ni kupeleka  vitamin A ambayo itapunguza  kiwango cha udumavu.

Nae Dkt.Beatrice Onyango amesema ndizi zinazotokana na  migomba hiyo zinavirutubisho vya vitamin A ila haiwezi kukinzana na ugonjwa wa mnyauko ambao umekuwa tishio kwa Migomba hapa nchini.

Bado mkoa wa kagera unakabiliwa sana na ugonjwa wa mnyauko wa migomba ,ugonjwa ambao umeduma pasipo kupata suruhisho la kudumu.

Post a Comment

0 Comments