habari Mpya


Usie Mfanyabiashara Mdogo Usiombe Kitambulisho -DC Mntenjele.

Tunataka mfanyabiashara ndogo ndogo ndiyo achukue kitambulisho; ambao tayari wana TIN na wanalipa kodi ya serikali wakigundulika wamepokea kitambulisho hiki, watachukuliwa hatua za kisheria.” Alisema Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele.

Mntenjele ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashra ndogondogo Disemba 31, 2018, katika viwanja vya Posta ya Zamani mjini Ngara.

Vitambulisho hivi havitatolewa kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara ya mtu, wala kwa watu wenye maduka yaani ambao wamepewa TIN ya kulipa mapato ya serikali, bali kwa wafanya biashara ndogo ndogo kwa kuzingatia maelekezo ya Rais.” Alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Lengo siyo kukwepesha watu wasilipe kodi; wale wenye uwezo wa kulipa kodi walipe na wale wadogo watalipa shilingi 20,000/= kadili ya maelekezo ya Mh. Rais, ili kuwaondolea bughudha ya kufukuzana na wanaokuja kuwadai kodi ya serikali.

Kwa hiyo, mfanyabiashara watakaotambulika kwamba ni wadogo ni wale ambao mauzo yao ghafi; yaani mauzo yao kwa siku hayo hayazidi shilingi 11,000/= na kwa mwaka mapato yao hayazidi milioni nne (4,000,000/=).

Malipo yanayotakiwa ni shilingi 20,000/= na wala hakuna ziada na malipo hayo ynafanyika benki mtu yeyote asije akakuomba fedha yoyote baada ya kulipia kitambulisho hicho; malipo yaliyotangazwa ni 20,000/=.” Alisema Mkuu wa Wilaya.

Hata hivyo, wale waliosajailiwa kulipa kodi ya serikali na wanabiashara kubwa, lazima walipe kodi kwa mtindo huo; na si kwa kujifanya wafanyabiashara wadogo, ili uweze wakwepe jukumu la kulipa kodi ya serikali.

Amsema ana taarifa kwamba kuna watu wanachukua biashara toka kwenye maduka ya watu na kupanga sokoni; na kuongeza kwamba ikiwa biashara hiyo siyo ya wafanyabiashara ndogo ndogo hawataruhusiwa kupata vitambulisho hvyo.

Amewasisitiza kujaza fomu maalumu inayopatikana kwa mkuu wa mkoa lakini kwa vile nafanyakazi kwa niaba ya mkuu wa mkoa, kwa hiyo fomu hizo zinapatikana ofisini kwa mkuu wa wilaya muda wote wa kazi.

Amewafafanulia kwamba fedha hiyo watailipa benki kwa kufuata utaratibu watakaopewa na TRA; na kuongeza kwamba wakisha lipa wataaleta stakabadhi kwa Katibu Tawala, ambaye atawapatia kitambulisho tayari waendelee na kazi.

Post a Comment

0 Comments