habari Mpya


''Tukikuta Mzazi Kaficha Mtoto Mlemavu Tutamshughulikia Ipasavyo''-DC Sengerema.

M.V. Sengerema.


Erick Ezekiel- RK Sengerema 90.5


Serikali wilayani Sengerema mkoani Mwanza imesema haitasita kuwachukulia hatua wazazi na walezi wanaowaficha watoto wenye ulemavu na kushindwa kuwapeleka shule kupata haki yao ya msingi ya elimu.

 Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Sengerema Bw. Emmanuel Kipole wakati akizungumzia mwitikio wa wazazi kuandikisha watoto wenye ulemavu katika shule maalum za walemavu wilayani humo.


Bw. Kipole amesema kuwa sheria ya elimu inamtaka kila mzazi kumpeleka mtoto shule bila kujali hali yake na kwamba serikali itaendesha msako wa kubaini wazazi ambao wanakaidi agizo la serikali la kuwapeleka shule watoto wenye ulemavu.

Naye Afisa Elimu Maalum wa Halmashauri ya Sengerema Bi. Kahabi Magesa amesema kuwa mpaka kufikia sasa wameweza kuboresha njia za walemavu wanaotumia kiti mwendo pamoja na vyoo na zaidi ya watoto 50 wenye ulemavu wamekwisha andikishwa ili kujiunga na shule kwa mwaka 2019.

Post a Comment

0 Comments