![]() |
Wafungaji wa
Simba katika mechi hiyo ni Cletus Chama
dakika 28 na 33, Emmanuel Okwi dakika 51
na Meddie Kagere dakika ya 63.
|
![]() |
Nacho Kikosi
cha Mtibwa Sugar, kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Northern
Dynamo katika mchezo wa marudio wa kombe la shirikisho Afrika uliochezwa katika
visiwa vya Shelisheli.
Bao la
Mtibwa lilifungwa na Haruna Chanongo
dakika ya 68 bada ya kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya bila kufungana.
Katika
mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Chamazi, Mtibwa walifanikiwa kushinda kwa
mabao 4-0 hivyo mzigo waliokuwa nao Dynamo leo ulikuwa mzito kuweza kufunga
mabao 5-0.
Kwa matokeo
hayo Mtibwa wanafanikiwa kusonga mbele katika hatua ya kwanza ya michuano hiyo
baada ya kufanikiwa kushinda mchezo wa leo ugenini.
|
0 Comments