habari Mpya


Shirika la FAO lasema Zao la Ndizi litaendelee kuwa zao Tegemezi la Chakula mkoani Kagera.

Mikungu ya ndizi ikiwa imekusanywa tayari kusafirishwa kwenda sehemu mbalimbali kwa ajili ya kupata soko, hata hivyo ndizi ambazo ndio lilikuwa zao kuu la chakula kwa wakazi mkoa wa Kagera kwa sasa uzalishaji wake umepungua huku bei yake zikipanda mara dufu  kutokana na migomba kuathiriwa na mnayuko.
Shirika la chakula duniani FAO limesema kuwa ili zao la Ndizi mkoani Kagera liendelee kuwa zao tegemezi la chakula mkoa humo ni lazima wakulima waelimishwe jinsi ya kupambana na magonjwa nyemelezi ya zaio hilo.


Afisa wa shirika hilo mkoani Kagera Bw Julias Onoko akizungumza na Redio Kwizera amesema zao la ndizi ni moja ya zao muhimu linalochangia kuingiza pato la taifa mkoani humo.


Amesema kwa siku za hivi karibuni zao hilo limeshambuliwa na magonjwa yanayochangia kupunguza uzalishaji.


BW.JULIAS ONOKO.

Kwa upande wao baadhi ya Wakulima wa migomba walio zungumza na Redio Kwizera wamesema upatikanaji wa mbegu bora na mbolea ni changamoto hivyo wameiomba serikali kutatatua changamoto hizo waweze kuzalisha kwa tija.

Post a Comment

0 Comments