habari Mpya


Rais Magufuli Agiza Kikokotoo cha Zamani Kitumike kuwalipa Wastaafu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania , Dkt.John Pombe Magufuli ameagiza kuwa kikokotoo kilichokuwa kinatumika kwa kila mfuko kabla ya Mifuko ya Hifadhi za Jamii kuunganishwa kiendelee katika kipindi cha mpito hadi mwaka 2023, kuwalipa Wastaafu ambapo wanachama 58,000 ndio Watastaafu katika kipindi hicho.

Rais Magufuli amesema hayo leo Disemba 28, 2018 alipokutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), vyama shiriki, watendaji wakuu wa mifuko ya Hifadhi ya jamii ya PSSSF na NSSF na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) ili kujadili kwa pamoja kuhusiana na mjadala wa kikokotoo kipya cha mafao kwa wastaafu.

Nimeamua kuwe na kipindi cha mpito, nimeamua kile kikokoto kilichokuwa kinatumika kwa kila mfuko kabla ya mifuko kuunganishwa, kiendelee kutumika katika kipindi cha mpito yaani hadi mwaka 2023” Rais Magufuli.

Kustaafu sio dhambi, Kustaafu ni heshima, huyu Mstaafu anatakiwa aheshimiwe, halafu unaanza kumpa 25% eti kwa kigezo kuwa itakusaidia kadri unavyoendelea kuishi, nani amekwambia nitaishi miaka mingapi” Rais Magufuli.

Post a Comment

0 Comments