habari Mpya


Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi yaongezeka Biharamulo.

Na Wiliam Mpanju -RK Biharamulo 97.9.

Maambukizi ya virusi vya UKIMWI  wilayani Biharamulo Mkoani Kagera  yameongezeka  kutoka asilimia 2.5 kwa Mwaka 2017  hadi kufikia  asilimia 3 kwa  mwaka 2018.
Mganga mkuu wa wilaya ya Biharamulo Dr Gabliel Mashauri amesema hayo wakati akieleza hali ya maambukizi hayo kwa wilaya ya Biharamulo katika kikao cha ushauri cha Wilaya hiyo kilichofanyika mjini Biharamulo.

Amesema  pamoja na maambulizi hayo  kuongezeka  idara ya  afya kupitia  kitengo cha kudhibiti Ukimwi  wanaendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kupima  afya kwa hiari.   
DR MASHAURI
Naye  mkuu wa wilaya ya Biharamulo  Bi Saada Malunde amesema  takwimu zinaonyesha  waliobainika kuwa na maambukizi  ya ugonjwa huo ni vijana  kuanzia miaka  20 hadi kufikia 35 hivyo ameutaka uongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo kutoa elimu  ya umuhimu wa kupima afya zao.

Post a Comment

0 Comments