habari Mpya


Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi yapungua Muleba.

Maambukizi ya virusi vya ukimwi katika halimashauri ya wilaya ya Muleba mkoani Kagera yamepungua kutoka asilimia 8 ya mwaka 2014 hadi kufikia asilimia 2.2 kwa mwaka huu,2019.

 Akisoma taarifa mratibu wa maambukizi ya virusi vya ukimwi wilaya ya Muleba Bi. Emirieta William katika maadhimisho ya siku ya ukimwi dunian December 01,2018 ambapo ki wilaya yamefanyika katika kata ya Nshamba. 

Bi. William amesema kuwa njia pekee walioitumia  kudhibiti maambukizi ya virusi vya ukimwi wameweza kutoa elimu kwenye vituo vya Afya na Zahanati na kufungua vituo vya kutolea huduma ambapo mpaka sasa wameweza kufungua  vituo 34.
Naye aliye mwakilisha mkuu wa wilaya ya muleba kama mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo Bw. Benard Kusekwa  amesema halimashauri hiyo imeweza kubaini watu wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi zaidi ya watu elfu 24482 huku kati ya hao zaidi ya watu elfu 22,979 wanapata dawa za kufubaza virus vya ukimwi.

Post a Comment

0 Comments