habari Mpya


Maadhimisho ya Krismasi 2018, Kitaifa yatafanyika katika Jimbo Kuu Katoliki Mwanza.

Image result for mwanza
Jiji la Mwanza -Radio Kwizera tupo hewani kupitia 97.7

Maadhimisho ya Sikukuu ya Krismasi 2018, Kitaifa yatafanyika katika Jimbo Kuu Katoliki Mwanza.

Taarifa ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) iliyotolewa na Mratibu wa Kurugenzi ya Mawasiliano, Pascal Mwanache imesema maadhimisho hayo yatatanguliwa na mkesha wa Krismasi utakaofanyika katika Kanisa Kuu la Epifania Bugando.

Misa ya mkesha itaongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Bunda ambaye pia ni msimamizi wa Kitume wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, Mhashamu Renatus Nkwande.

Aidha misa takatifu ya Krismasi Desemba 25, 2018 itakayoanza saa nne kamili asubuhi itafanyika katika kanisa la Epifania Bugando na pia itaongozwa na Askofu Renatus Nkwande,” imesema taarifa hiyo.

Baraza hilo limewaalika waumini wa dini hiyo kuungana katika kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo ambaye ni mkombozi wa ulimwengu.SOMA TAARIFA KAMILI HAPA CHINI.

Post a Comment

0 Comments