habari Mpya


Kazilantemwa FC yaishinda Bureza FC 2-0 Ufunguzi Ligi ya Breza Cup 2018.

Timu ya Kazilantemwa FC imeibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 0 dhidi ya  timu ya Bureza FC kwenye ufunguzi wa Ligi ya Breza Cup 2018 iliyofunguliwa Al hamisi December 13, 2018, katika uwanja wa Ndangara Stadium.
Magori ya Kazilantemwa FC yamefungwa na  Mozarius Sevelin dakika ya 4 na Muksini Alikadi dakika ya 32 huku ligi hiyo ikitarajiwa kuendelea  Leo December 14,2018 baina ya Butembo FC na Makarwe FC.

Muandaaji wa Ligi hiyo  Morisoni Samweli amesema lengo ni nikuweka amani katika kata hiyo huku jumla ya timu 4 zikishiriki ligi hiyo ambazo ni Bureza FC, Kazilantemwa FC , Makarwe FC na Butembo FC.

Mshindi wa kwanza atajinyakulia mbuzi mnyama, mshindi wa pili atajinyakulia kitita cha shilingi elfu thelathini na ligi hiyo inatarajiwa kumalizika December 25 mwaka huu.
Mwanahabari wetu Shafiru Yusuph na Taarifa kutoka Uwanja wa Ndagara, wilayani Muleba mkoani Kagera.

Post a Comment

0 Comments