habari Mpya


Kaigara yaanza Upasuaji Wagonjwa.

Na Shafiru Yusuf -RK Muleba 97.9

Kituo cha Afya cha Kaigara kilichopo Wilayani Muleba Mkoani Kagera kinatarajia kupunguza vifo vya kina mama na mtoto baada ya kuanza hatua ya upasuaji.

 Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho, Bw. Alibert Bongo amesema hatua ya kupasuji imeanza toka December 15, 2018 ambapo wameweza kupasua wa kina mama wajawazito wawili na wako salama hadi sasa.

Bw. Bongo amesema kuwa kwa sasa kituo hicho kina uwezo wa kuhudumia wagonjwa wanne kwa siku kwa ajili ya upasuaji  kwani awali walikuwa wanawapeleka katika hospitali teule ya wilaya hiyo ya  Rubya kwa ajili ya matibabu.
Naye Mganga Mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt Mondest Rwakahemula amesema kuwa kituo hicho ni kituo pekee kinachofanya upasuaji katika wilaya hiyo kati ya vituo vya Afya Vitano vilivyopo wilayani humo.

Post a Comment

0 Comments