habari Mpya


Kagera Kutangazwa na Utalii Wanyamapori Katika Mapori ya Kimisi, Burigi na Biharamulo.

Baadhi ya Twiga wanaopatikana katika Pori la Akiba Burigi.

Imeelezwa kuwa kuongezeka kwa wanyamapori wa kila aina katika mapori ya Kimisi, Burigi na Biharamulo ni sehemu ya kuutangaza mkoa  wa Kagera  kitaifa na kimataifa kupitia  watalii watakaofika kutembelea wanyama hao.


Afisa wanyama pori wa Burigi, Kimisi na Biharamulo BI. WINNE KWEKA ameiambia radio Kwizera kuwa mapori hayo yamepandishwa hadhi na kuwa ya hifadhi ya Taifa ambayo ni matokeo ya kuongezeka kwa wanyama pori.

Amesema miongoni mwa wanyama pori maarufu waliongezeka katika mapori hayo ni pamoja na makundi ya Simba, Faru, Tembo, Twiga, Nyati ,Chui na ndege wa kila aina.
Ndege aina mbalimbali pia ni kivutio katika pori hilo.

Naye Meneja Hifadhi ya Wanyama pori katika  mapori hayo BW BIGILAMUNGU  KAGOMA  amesema  wameshaanza kutoa elimu kwa wananchi wanaozunguka mapori hayo ili kuweka tahadhari na kwamba watoe taarifa kwa viongozi wa vijiji pale watakapoingia kwenye makazi na mashamba ya watu. 

Post a Comment

0 Comments