habari Mpya


Jamii inawajibika Kuzuia Vifo vya Wajawazito na Watoto.

Bi.Martha Shakinyau akiongea na Wanahabari Mkoani Kigoma ambao hawapo Pichani.

Na Adrian Eustace-  RK Kigoma 94.2

Wizara ya  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kitengo cha afya ya uzazi na watoto kwa kushirikiana na ofisi za Waganga Wakuu wa Mikoa ya Kigoma na Tabora inayounda Kanda ya Magharibi imeendesha kikao kazi cha wadau mbalimbali wa afya kutoka mikoa hiyo lengo likiwa ni kuweka mikakati ya kupunguza kasi ya vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga.

Aidha imeelezwa kuwa hali ya vifo kwa wajaa wazito kitaifa ni vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,00  huku takwimu zikionesha kuwa jumla ya vifo 25 kwa kila vizazi hai 1,000 vinatokea kwa watoto wachanga.

Mratibu wa Kitaifa wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto kutoka Wizara ya Afya Bi.Martha Shakinyau amesema vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga havikubariki na kwamba kila mwanajamii anawajibika kutoa taarifa mapema pindi anapobaini dalili hatarishi kwa mama mjamzito ili afikishwe kwenye kituo cha afya kabla madhara zaidi hajajitokeza.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Paul Chaote amesema hali ya vifo vya wajawazito na watoto kwa mkoa huo imepungua ikilinganishwa na kipindi cha nyuma na kwamba hali hiyo imetokana na jitihada za Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa elimu kwa jamii na watoa huduma za afya kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments