habari Mpya


Halmashauri ya wilaya ya Ngara ya pokea shilingi bilioni 13.2 kutekeleza miradi ya maendeleo.

Ngara Kagera na Shaaban Ndyamukama.  
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali  Marco Gaguti, ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Ngara, kusimamia miradi ya LADP  na kufanya kazi kwa msimamo , uandilifu na umakini ili kuwaletea manufaa  walengwa wilayani humo.

Brigedia Jenerali Marco  Gaguti ametoa agizo hilo wakati akipokea taarifa ya viongozi wa wilaya hiyo juu ya  utekelezaji wa miradi ya kijamii baada ya benki ya dunia kutoa  mkopo wa Sh13.2 bilioni  kupitia miradi ya Local Area Development Plan (LADP).

Awali Mratibu wa mpango wa maendeleo vijijini LADP Herman Hume amesema baada ya kuanza  ujenzi wa miradi mbalimbali katika maporomoko ya mto Rusumo mpakani na nchi ya Rwanda  wakazi wa wilaya ya Ngara watanufaika.
Hume amesema fedha hizo dola 668 za kimarekani sawa na Sh13.2 bilioni zitatumika kuboresha miundombinu katika sekta ya Afya, elimu, maji   kilimo na mifugo ikiwa ni pamoja na kuendeleza vikundi vya ujasiriamali  


Amesema  kiasi cha Sh2.8 bilioni kinatarajia kutekeleza mradi wa maji katika  kijiji cha Rusumo  na vijiji vingine  vinne vya Mshikamano, Kasharazi  Rwakalemela, na Kasulo vimetengewa Sh1.12 bilioni.
Vile vile amesema halmashauri ya wilaya hiyo, inaendesha chuo cha maendeleo ya jamii Lemala hivyo kupitia fedha hizo kitaboreshewa mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa kununua vifaa vya aina mbali mbali ya  ufundi vinavyohitajika
 

Amesema  Sh280 milioni zitajenga Zananati mpa katika  kijiji cha Kyenda lakini pia   shule mpya ya msingi  Rusumo  na zaidi ya Sh4 bilioni zitaboresha miundombinu katika kituo cha Afya Lukole ,shule  za sekondari Bukiriro  Nyamiaga na shule ya msingi Makugwa iliyoanzishwa kata ya Mugaza.
“Miundombinu itakayoboreshwa ni pamoja na vyumba vya madarasa, mabweni ofisi, nyumba za watumishi,majengo ya utawala lakini hata matundu ya vyoo lengo ni  wananchi kupunguza changamoto zinazowakabili” Amesema Hume.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Ngara Luteni Kanali  kanali Michael Mntenjele ameahidi kusimamia miradi iliyoainishwa  inatekelezwa  ilivyopangwa na kwamba    watanzania kadhaa wameajirawa katika miradi ya maporomoko ya Mto Rusumo kunakojengwa mradi wa Umeme wa nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi

Post a Comment

0 Comments