habari Mpya


Fahamu Hali ya HIV/Ukimwi mkoani Kagera.

Januari hadi Oktoba mwaka huu,2018 mkoa wa Kagera waliojitokeza kupima afya zao walikuwa watu milioni 1.3 kati yao  watu 16,048 walikutwa na maambukizi sawa na asilimia 1.2.

Kutoa elimu kuhusu namna ya kuepuka ugonjwa huo, mkoa wa Kagera umefanikiwa kupunguza maambukizi kutoka asilimia 1.6 kwa mwaka 2017.

Taarifa ya mkoa wa Kagera imeeleza kuwa Wilaya ya Misenyi ina Maambukizi ya asilimia 1.8, Ngara  asilimia 0.5, Muleba asilimia1.7 , Biharamulo asilimia1.0 Bukoba Vijijini asilimia 1.7  Bukoba Manispaa asilimia1.7 ,hivyo Jamii kutakiwa kuwa na uaminifu katika  ndoa zao. 

Katika kampeni ya Furahisha ya  mkoani Kagera iliyofanyika September,2018, watu waliojitokeza kupima  walikuwa 741 kati yao wanawake walikuwa 349, wanaume 392 waliokutwa na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ni  wanaume watatu na wanawake watano.

Aidha,Shirika la afya duniani WHO linasema, watu Milioni 37 duniani, wanaishi na maambukizi ya ukimwi huku vijana wakiendelea kuwa hatarini zaidi kuambukizwa hasa barani Afrika.

Pia Watu wengine Milioni 22 walioambukizwa, wanatumia dawa ya AVRs ambayo imesaidia watu wengi sana kuendelea kuishi.

Post a Comment

0 Comments