habari Mpya


DCP Ahmed Msangi Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amembadilisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi kuwa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na Msemaji wa Jeshi hilo.


Kamanda Msangi amechukua nafasi ya Barnabas Mwakalukwa ambaye ameteuliwa kuwa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Pwani.

Aidha, Jeshi la Polisi nchini limewataka wananchi wote kutii Sheria bila shuruti katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka na kusema hakuna atakayekuwa salama endapo atavunja sheria za nchi.


BOFYA HAPA CHINI KUMSIKILIZA KAMANDA MSANGI.
Ameongeza kuwa Takwimu za Makosa ya Jinai zimetajwa kupungua kutoka laki 4 elfu 96 na 677 kuanzia mwezi Januari hadi Oktoba mwaka 2017 na kufikia laki 4 elfu 89 na 429 mwezi Januari hadi Oktoba mwaka huu,2018 ambayo inatajwa kua ni pungufu ya makosa elfu 7 na 248 sawa na asilimia 1.5.

Post a Comment

0 Comments