habari Mpya


DC Buhigwe Aagiza Viongozi na Wananchi Kutatua Mgogoro Ardhi Kijiji cha Kishanga.

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Luteni Kanal Michael Masala Ngayalina Amefanya ziara yake ya kwanza katika kutekeleza na kusikiliza kero za wananchi katika ngazi za Kata na Vijiji.

Na Albert Kavano -RK Buhigwe 94.2
Katika ziara hii alizungumzi maendelo ya wananchi katika nyanja mbali mbali ikiwemo kuwaagiza wananchi na viongozi wa kijiji cha Kishanga wilayani humo kumaliza mgogoro wa eneo lililotengwa kwa ajili ya huduma za jamii unaokwamisha huduma za jamii.

Mgogoro wa ardhi ulio kati ya wananchi na serikali ya kijiji hicho umedumu kwa miaka minne tangu kutengwa kwa hekari sitini na tano kwa ajili ya miundombinu ya Shule, Soko na Zahanati.

Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Luten Kanal Michael Masala Ngayalina ameagiza viongozi wakae kutatua mgogoro huo bila kujali itikadi za Kisiasa

DC L.KANAL NGAYALINA
Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wamesema baada ya kutengwa kwa eneo hilo kwa ajili ya huduma za jamii wengi wameathirika kwa kukosa maeneo ya kulima hivyo wameling’ang’ania eneo hilo kwa kutaka kupata eneo mbadala la kufanya shughuli za kilimo.

Post a Comment

0 Comments