habari Mpya


CRDB Banki Yasaidia Madawati Wilayani Kasulu.


Wanafunzi wa Shule ya msingi Juhudi ya mjini Kasulu mkoani Kigoma (walioka kulia) wakiwa na Meneja wa CRDB Tawi la Kasulu, Paul Chacha (kushoto) wakipokea madawati kutoka Benki ya CRDB tawi la Kasulu mkoani Kigoma yaliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya wanafunzi wa Shule yao.Na Philmon Golkanus -RK Kasulu 94.2Shule ya msingi Juhudi iliyopo mjini Kasulu mkoani Kigoma inakabiliwa na uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa na kusababisha changamoto kubwa ya utoaji huduma bora ya elimu.Shule hiyo yenye jumla ya Wanafunzi 4,993 ina uhitaji wa madawati 1,400 ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi lakini hadi sasa ina madawati 400 pekee na upungufu wa madawati 1000.

Katika kupunguza tatizo hilo Bank ya CRDB Tawi la Kasulu,mkoani Kigoma kupitia kwa Meneja wake Bw. Paul Chacha , amekabidhi madawati 50 kwa shule hiyo, kama sehemu ya faida inayotokana na wanajamii wanaotumia Benki hiyo.Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Twalibu Ismail akipokea madawati hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri ya mji huo Bi.Fatina Laay ameishukuru CRDB kwa mchango huo na  kuomba taasisi na mashirika mengine kuwasaidia kuondokana na changamoto hizo.

Post a Comment

0 Comments